Sheria na HakiColombia
Colombia yaongoza kwa mauaji ya wanaharakati wa mazingira
13 Septemba 2023Matangazo
Katika ripoti yake ya kila mwaka, shirika hilo lenye makao yake mjini London, Uingereza limesema mauaji dhidi ya wanaharakati wa mazingira yameongezeka maradufu nchini Colombia mwaka jana, huku ikitoa orodha ya watetezi 177 wa ardhi na mazingira ambao waliuawa mwaka 2022 kuanzia Ufilipino hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Idadi ya waliouawa imepungua kidogo ukilinganisha na rekodi ya watu 227 waliouawa mwaka 2020, lakini shirika la Global Witness limesema hii haimaanishi kuwa kwa kiasi kikubwa hali imeboreka.
Shirika hilo limesisitiza kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za kilimo, mafuta na madini kutazidisha shinikizo kwa mazingira pamoja na wanaharakati wanaohatarisha maisha yao ili kuilinda sayari.