1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiColombia

Colombia:Watu wahamishwa kufuatia hatari ya Volkano

7 Aprili 2023

Colombia inaendelea na zoezi la kuwahamisha watu 2,500 wanazoishi karibu na Volkano ya Nevado del Ruiz inayofuatiliwa kwa karibu kutokana na uwezekano wa mripuko, lakini baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamekataa kuondoka.

https://p.dw.com/p/4PogS
BdT Kolumbiens höchster Vulkan ausgebrochen
Picha: picture-alliance / dpa

Serikali ya Colombia imeongeza kiwango cha tahadhari kufuatia kuongezeka kwa mitetemeko ya ardhi inayoashiria uwezekano mkubwa wa mripuko wa volkano katika siku ama wiki  zijazo. Rais Gustavo Petro, ameagiza zoezi hilo la uhamishaji kuharakishwa.

Karibu watu 57,000 wanaishi katika jumla ya miko sita iliyopo katika eneo lenye hatari la volkano. Mripuko wa volcano wa mwaka 1985 ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 25,000, ikiwa ni janga kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Colombia.