City yaitandika Bayern na kusonga mbele ligi ya mabingwa
20 Aprili 2023City wametinga hatua ya nusu fainali na sasa watakwaana na Real Madrid. Awali Haaland ambaye ni mzaliwa wa Norway alikosa mkwaju katika dakika ya 37 lakini hakukata tamaa na hatimaye kupachika bao la kwanza mnamo dakika ya 57 mara baada ya Bayern kukosa kutumia vema nafasi waliyoipata.Mabingwa watetezi Real Madrid waishinda Chelsea 2-0
Bayern walikosa kujiamini baada ya kupoteza mechi ya kwanza kwa mabao 3-0. Manchester ilionekana nayo kama imeshindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata. Joshua Kimmich alifunga bao la nguvu la Bayern kwa mkwaju wa penalti dakika ya 83 baada ya beki wa City Manuel Akanji kuadhibiwa kupitia VAR kwa mpira wa mikono.
Mchezaji mwenzake wa Bayern Dayot Upamecano pia aliadhibiwa kwa mpira wa mikono wakati pasi ya Ilkay Gündogan iliposhika sehemu ya chini ya mkono wake dakika ya 35, lakini Haaland alibutua mkwaju huo juu ya goli.
Hiyo ni mara ya tatu mfululizo kwa Bayern kuondoshwa katika hatua ya robo fainali tangu ishinde michuano hiyo mwaka wa 2020 na shindano la pili kutolewa ndani ya wiki kufuatia ushindi wa Freiburg dhidi ya Bayern katika robo fainali ya Kombe la Ujerumani.
Kocha wa Bayern, Thomas Tuchel alitolewa nje na kadi yake ya pili ya njano kwa ulalamishi, huku msaidizi wake Zsolt Löw akionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. City inawania kushinda ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza. Itakuwa mara ya kwanza kwa Guardiola kushinda akiwa na City tangu ashinde kama kocha wa Barcelona mwaka 2011. Bruce Amani kutoka dawati la michezo anaitathmini mechi hii na kuangushwa kwa Bayern