TeknolojiaIndia
Chombo cha anga za juu cha India kujaribu kutua mwezini
23 Agosti 2023Matangazo
Chombo hicho kinatazamiwa kugusa ardhi ya ncha ya kusini ya mwezi majira ya saa tisa alasiri kwa saa za Afrika Mashariki. Jaribio kama hilo la India la mnamo mwaka 2019 lilishindwa na chombo kilichotumwa wakati huo kilianguka.
Mkuu wa Shirika la Anga za Mbali la India, K.Sivan, amesema picha za hivi karibuni zilizotumwa na chombo kinachotarajiwa kutua mwezini zinatoa ishara kuwa jaribio la leo litafanikiwa.
Jaribio hilo la India linafanyika siku chache tangu chombo cha Urusi kilichotumwa mwezini kuanguka na kusambaratika kilipokuwa katika hatua za mwisho za kujaribu kutua kwenye satelaiti hiyo ya asili iliyo umbali wa kilometa 384,000 kutoka duniani.