China yawashinikiza wabunge kutoka nchi 6 dhidi ya Taiwan
28 Julai 2024Wanasiasa kutoka Bolivia, Colombia, Slovakia, Macedonia Kaskazini, Bosnia na Herzegovina, na nchi nyingine moja kutoka Asia ambayo haikutaka kutambulishwa, wamesema wamekuwa wakipokea ujumbe, simu na maombi ya dharura kwa mikutano ambayo ingekinzana na mipango yao ya kusafiri kuelekea Taiwan, kwa kile wanachoelezea kuwa ni juhudi za kukitenga kisiwa hicho kinachojitawala.
Mkutano wa Taiwan ni wa Muungano wa Mabunge kuhusu China
Mkutano huo unaanza kesho Jumatatu na unafanywa na Muungano wa Mabunge kuhusu China, kundi la mamia ya wabunge kutoka nchi 35 wanaojihusisha na jinsi mataifa ya kidemokrasia yanavyoshirikiana na China.
Taiwan ina uhusiano usio rasmi na nchi nyingi
Mara kwa mara China imekuwa ikitishia kulipiza kisasi dhidi ya wanasiasa na nchi zinazoonyesha kuiunga mkono Taiwan, ambayo ina uhusiano usio rasmi na nchi nyingi kutokana na shinikizo la kidiplomasia laChina.