China yaunga mkono Somalia kulinda mamlaka na mipaka yake
12 Januari 2024China imetoa wito wa kuheshimiwa mipaka ya Somalia, baada ya makubaliano ya baharini yaliyofikiwa baina ya Ethiopia na jimbo linalojitawala la Somaliland kuzusha mvutano wa kikanda.Rais wa Somalia afuta mkataba wa Somaliland na Ethiopia
Katika ujumbe uliochapishwa kwenye ukurasa wa X wa ubalozi wa China nchini Somalia, ulisema kuwa Somaliland ni sehemu ya Somalia na kwamba China inaunga mkono serikali ya shirikisho ya Somalia katika kulinda umoja, mamlaka na uadilifu wa mipaka yake.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Pembe za Afrika, IGAD ilisema jana kuwa itakutana Januari 18 nchini Uganda kujadili mvutano kati ya Ethiopia na Somalia, pamoja na hali ya Sudan, ambayo imekumbwa na mapigano tangu mwezi Aprili baina ya majenerali hasimu.
Marekani, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya nchi za kiarabu, Misri na Uturuki tayari zimetoa wito wa kuheshimu mamlaka ya Somalia.