China yaihimiza EU kuhusu bahari ya China Kusini
2 Septemba 2024Taarifa ya ubalozi wa China katika Umoja wa Ulaya imesema China haijaridhishwa na madai ya Umoja huo dhidi yake kuhusu suala hilo. Taarifa hiyo imesema Umoja wa Ulaya si mdau katika suala la bahari ya China Kusini na haina haki kutoa lawama kuhusu suala hilo.
China na Ufilipino zilituhumiana kwa kugongesha makusudi vyombo vya walinzi wa pwani katika maeneo ya bahari ya China Kusini yanayozozaniwa Jumamosi iliyopita.
Kugongana huko kwa vyombo hivyo karibu na eneo la Sabina ni tukio la tano la malumbano ya baharini katika kipindi cha mwezi mmoja katika uhasama wa muda mrefu kuhusiana na njia hiyo muhimu ya majini.
Umoja wa Ulaya ulisema jana Jumapili kwamba unalaani vitendo hatari vya vyombo vya walinzi wa pwani wa China dhidi ya operesheni halali za Ufilipino katika bahari hiyo.