1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yatoa wito wa kusitishwa vita vya Gaza

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

China inasema inataka vita vya Israel na Hamas vikomeshwe mara moja, ikitangaza kuwa iko tayari kufanya kazi na serikali za mataifa ya Kiarabu kwa ajili ya kusaka suluhu ya kudumu katika mzozo huo unaondelea kufukuta.

https://p.dw.com/p/4Xjov
China  Xi Jinping
Rais Xi Jinping wa China.Picha: Kyodo/picture alliance

Rais Xi Jingping wa China amesema hayo leo Alkhamis, baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly.

Madhouly alikuwa mjumbe mkuu pekee kutoka Mashariki ya Kati kuhudhuria Kongamano la Miundombinu ya Usafiri la China na kuongeza kuwa ni lazima kusitisha mapigano hayo haraka iwezekanavyo ili kuzuwia mzozo huo kuenea au kutoka nje ya udhibiti.

Soma zaidi: Israel na kundi la Islamic Jihad wakubali kusitisha mapigano

Haya ni matamshi ya kwanza ya Rais Xi kuyatoa kuhusu mzozo huo uliozuka baada ya Hamas kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7 kulikofuatiwa na mashambulizi makubwa ya kijeshi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.