1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

China yatoa wito wa kuanzishwa tena usafirishaji wa nafaka

22 Julai 2023

China imezitolea wito Ukraine na Urusi kuharakisha kuanza tena mazungumzo ya usafirishaji wa nafaka.

https://p.dw.com/p/4UG6k
Themenpaket | Getreidehandel Getreide-Deal Grain deal Ukraine Russland
Picha: FEISAL OMAR/REUTERS

Wito huo umetolewa ikiwa ni siku chache tangu Urusi ilipojiondoa kwenye mkataba wa kimataifa wa usafirishaji wa bidhaa za kilimo kupitia Bahari Nyeusi.

Soma pia: Athari za uamuzi wa Urusi kujiondoa katika mpango wa usafirishaji nafaka

Msaidizi wa mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, Geng Shuang ameyasema hayo jana Ijumaa wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jijini New York.

Shuang ameongeza kuwa, Beijing inatumai kwamba pande husika katika mvutano huo zitafanya kazi na vyombo vya Umoja wa Mataifa ili kupata suluhisho.

Aidha mwakilishi huyo amesema kufufua mazungumzo hayo ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula katika ngazi ya kimataifa.

Uamuzi wa Urusi wa kujitoa kwenye mkataba huo wa usafirishaji wa nafaka Jumatatu ya wiki hii umesababisha mkwamo mpya wa shughuli za uchukuzi kwenye ujia wa Bahari Nyeusi.