China yatoa tahadhari ya mvua kubwa mjini Beijing
29 Julai 2023Mamlaka ya hali ya hewa ya China imetoa tahadhari ya mvua kubwa katika mji mkuu wa Beijing, na maeneo ya karibu. Tahadhari hiyo imetolewa wakati kimbunga Doksuri kikipiga maeneo ya bara na kusababisha hali mbaya ya hewa katika maeneo mengi ya nchi hiyo.
Kimbunga hicho kilipiga kusini mwa mkoa wa Fujian Ijumaa asubuhi kwa kasi ya kilometa 175 kwa saa.
China imekuwa ikikabiliwa na hali mbaya ya hewa na kurekodi kiwango cha juu cha joto kilichovunja rekodi katika msimu huu, jambo ambalo wanasayansi wanasema linasababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya China, wataalamu wameonya kuwa huenda mvua ya Jumamosi ikasababisha mafuriko mabaya zaidi ya yale ya Julai 2012 yaliyosababisha vifo vya watu 79 na kuhamishwa kwa maelfu ya watu.