1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yashindwa kumtuma waziri wake wa nje Indonesia

11 Julai 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang hatohudhuria mkutano wa kidiplomasia utakaofanyika Indonesia wiki hii kutokana na sababu za kiafya.

https://p.dw.com/p/4Tiqa
Indonesien ASEAN Gipfel
Picha: Achmad Ibrahim/AP Photo/picture alliance

Msemaji katika wizara hiyo Wang Wenbin ameeleza kuwa badala yake mwanadiplomasia mkuu Wang Yi ataiwakilisha China kwenye mkutano huo wa Jakarta.

Soma zaidi: Indonesia yaridhishwa na ushirikiano wa China kwa amani ya Myanmar
Widodo: ASEAN haipaswi kuwa wakala wa dola yoyote

Mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya ya kusini mashariki mwa Asia (ASEAN) na China wanatarajiwa kukutana mnamo siku ya Alhamisi, siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa jumuiya ya Asia ya Mashariki EAS na ASEAN.

Qin, mwenye umri wa miaka 57, alichukua nafasi ya Wang kama waziri wa mambo ya nje wa China mwezi Disemba na alionekana mara ya mwisho mbele ya umma Juni 25 mjini Beijing baada ya mkutano na maafisa kutoka Sri Lanka, Urusi na Vietnam.