China yasema Beijing inapendelea ushirikiano na Ujerumani
20 Juni 2023Matangazo
Li Qiang ameyasema hayo mjini Berlin muda mfupi baada ya kupokelewa na rais Frank-Walter Steinmeier kuanza ziara rasmi nchini Ujerumani.
Qiang ambaye ziara yake nchini Ujerumanni ni kwanza tangu alipoteueliwa kushika wadhifa huo amesema anatumai kuona ishara dhahiri za kuwepo sekta imara ya viwanda kimataifa pamoja na amani duniani.
Amesisitiza kwamba China iko tayari kufanya kazi pamoja na Ujerumani kuzika tofauti za kimtazamo zilizopo na kuimarisha mahusiano.
Hapo jana jioni Qiang alikaribishwa dhifa ya chakula cha jioni na kansela Olaf Scholz na hii leo anatarajiwa kushiriki awamu ya saba ya mashauriano ya kiserikali kati ya China na Ujerumani.