1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yasaini mikataba ya miundombinu na nchi za Afrika

5 Septemba 2024

China imetia saini mikataba kadhaa na Chad na Senegal inayohusisha miradi ya umeme, miundombinu na teknolojia ya mawasiliano.

https://p.dw.com/p/4kIiu
Mawaziri wa Tanzania wakisaini mikataba kati ya nchi yao na China
Mawaziri wa Tanzania wakisaini mikataba kati ya nchi yao na ChinaPicha: Tanzania presidential communication unit

Mikataba hiyo imesainiwa pembezoni mwa mkutano wa kilele kati ya China na Afrika mjini Beijing.

China ambayo ni mkopeshaji mkubwa zaidi duniani, imeyaalika mataifa 50 ya Afrika ikilenga kurekebisha uhusiano wake na nchi zinazoendelea kiuchumi.

Miradi ya Chad itahusisha uboreshaji wa miundombinu ya umeme na maji salama ya kunywa katika mji mkuu wa N'Djamena na ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa ndege nje ya mji huo.

Katika taarifa tofauti, Ofisi ya rais wa Senegal ilisema kuwa nchi hiyo imetia saini takriban mikataba kumi na mbili na China, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya habari na mawasiliano, masuala ya mazingira na vyombo vya habari.

Wakati huohuo China pia imetia saini makubaliano ya awali na Tanzania na Zambia kuhusu mradi wa reli.

Rais Xi Jinping alishuhudia utiaji saini wa mkataba huo juu ya ujenzi wa reli ya Tanzania kwenda Zambia (TAZARA).

Marais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na wa Zambia Hakainde Hichilema wapo mjini Beijing kuhudhuria Kongamano la Ushirikiano kati ya China na bara la Afrika.