1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yalenga kuongeza bajeti yake ya matumizi ya kijeshi

5 Machi 2023

China inapanga kuongeza bajeti yake ya matumizi ya kijeshi kwa asilimia 7.2 mwaka huu, kukabiliana na wasiwasi wa siasa za kikanda.

https://p.dw.com/p/4OHAX
China Peking | Nationaler Volkskongress - Li Keqiang
Picha: Ju Peng/AP/picture alliance

 Hayo yamebainika kupitia rasimu ya bajeti iliyowasilishwa katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa kila mwaka wa  bunge la umma wa  China mjini Beijing. 

Waziri mkuu anayeondoka Li Keqiang amewaambia wajumbe kiasi 3000 katika ukumbi mkuu wa bunge hilo kwamba wasiwasi umeongezeka katika mazingira ya nje. 

Ametowa mwito wa kutanuliwa  jeshi la ulinzi la taifa ambalo amesema linapaswa kuwa na kile alichokiita utayari wa kuimarisha mapambano na kuongeza uwezo wa kijeshi ili kufikia malengo waliyopewa na chama na umma wa China. 

Wafuatiliaji wamezungumzia wasiwasi wao kuhusu ongezeko la nguvu za kijeshi la nchi hiyo kwa kuzingatia kitisho chake kuelekea kisiwa cha Taiwan.