1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaapa kulinda maslahi yake baada ya kitisho cha Trump

22 Januari 2025

China imeapa kulinda maslahi yake ya kitaifa baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema kwamba ushuru wa forodha wa asilimia 10 kwa bidhaa za China unaweza kuanza kutekelezwa kuanzia Februari mosi.

https://p.dw.com/p/4pSRo
China  Mao Ning Beijing
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao NingPicha: Kyodo News/IMAGO

China imetangaza Jumatano kuwa italinda maslahi yake ya kitaifa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza kwamba ushuru wa forodha wa asilimia 10 kwa bidhaa za China ungetekelezwa kuanzia Februari mosi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, alifafanua msimamo huo akisema kwamba taifa hilo linaamini hakuna mshindi katika vita vya kibiashara au ushuru, hivyo litaendelea kulinda maslahi yake.

Soma pia: China yaonya vita vya biashara na Umoja wa Ulaya

Aidha, Trump alieleza kuwa kuna haja ya kurekebisha uwiano wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, akidai umoja huo haununui bidhaa za kutosha za Marekani, na hivyo angetafuta suluhisho kwa kuongeza ushuru au kuishawishi Ulaya kununua zaidi mafuta na gesi kutoka Marekani.