1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China, Ufilipino zagongana Bahari ya Kusini

22 Oktoba 2023

China na Ufilipino zimeshutumiana kufuatia mgongano uliotokea katika eneo linalozozaniwa la Bahari ya Kusini mwa China wakati boti ya China ilipoizuwia ya Ufilipino iliyokuwa inawapeleka wanajeshi wake huko.

https://p.dw.com/p/4Xs09
Meli za China na Ufilipino kwenye makabiliano katika Bahari ya Kusini mwa China siku ya Jumapili (Oktoba 22).
Meli za China na Ufilipino kwenye makabiliano katika Bahari ya Kusini mwa China siku ya Jumapili (Oktoba 22).Picha: Armed Forces of the Philippines/AP/picture alliance

Kukabiliana kwa wanajeshi wa majini wa pande hizo mbili siku ya Jumapili (Oktoba 22) ni mvutano wa hivi karibuni zaidi katika msururu wa mivutano katika bahari hiyo. 

Mataifa hayo yamekuwa yakizozania udhibiti wa maeneo ya Bahari ya Kusini mwa China na hasa katika eneo la Thomas Shoal ambalo ni sehemu ya visiwa vya Spratly.

Soma zaidi: Ufilipino na washirika wake kama Marekani na Uingereza wanataka kuonyesha nguvu za kijeshi katikati ya mvutano wa kikanda

Ufilipino ilikuwa ikiwapelekea vifaa wanajeshi wake walioko katika meli ya zamani iliyotumiwa katika Vita vya Pili vya Dunia, hatua iliyoilazimu China kuingilia kati na kuzuwiya operesheni hiyo.