China na Japan zathibitisha uhusiano wa kimkakati
17 Novemba 2023Matangazo
Wamesema hayo wakati wa mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana mwaka huu, ishara kwamba mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi barani Asia yanajaribu kuboresha uhusiano wao wenye matatizo.
Rais Xi alimwambia Kishida kwamba nchi hizo mbili zinapaswa kuzingatia maslahi ya pamoja na zithibitishe uhusiano wao wa kimkakati kwa manufaa ya pande zote mbili.
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alisema alimwelezea Rais Xi Jinping wasiwasi wake mkubwa kuhusu shughuli za kijeshi za China karibu na Japan, ikiwa ni pamoja na ushirikiano wake na Urusi.
Walisema hayo wakati wa mkutano wao wa pembezoni mwa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC).