China, Marekani kuzungumzia suala la Taiwan
26 Januari 2024Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin, aliwaambia waandishi wa habari kuwa Wang Yi angelielezea msimamo wa China juu ya uhusiano kati ya Beijing na Washington na kubadilishana mawazo juu ya masuala la kimataifa na kikanda.
Marekani ilieleza kuwa mazungumzo kati ya maafisa hao wawili yalitarajiwa kufanyika Alkhamis (Januari 25) na Ijumaa (Januari 26).
Soma zaidi:
Beijing na WashXi Jinping na Fumio Kishida walifanya mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa kilele wa APEC, mjini San Francisco, nchini Marekani
ington zimekuwa zikivutana katika miaka ya hivi karibuni kuhusu masuala ya teknolojia, biashara na haki za binaadamu pamoja na kisiwa cha Taiwan chenye utawala wa ndani na ushindani wao katika Bahari ya Kusini ya China.
Rais Joe Biden alikutana na mwenzake wa China, Xi Jinping, mjini San Francisco mnamo mwezi Novemba kwa mazungumzo ambayo pande zote mbili zilielezea kwamba yalikuwa na mafanikio