China 'kuimarisha ushirikiano wa kimkakati' na Urusi
9 Aprili 2024Wang ameyasema haya alipokutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov aliye katika ziara ya siku mbili nchini China kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia huku vita vya Urusi nchini Ukraine vikiendelea.
Kulingana na shirika la habari la RIA Novosti, Beijing na Moscow zitaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika jukwaa la dunia.
Simu ya Rais Xi wa China kwa Zelensky ina tija gani?
Lavrov, ameishukuru China kwa "msaada" wake baada ya kuchaguliwa tena kwa Rais Putin hivi majuzi, akitaja kwamba rais Xi Jinping alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutuma pongezi kwa rais Putin.
Marekani hivi karibuni imeionya Beijing dhidi ya kutoa misaada isiyo ya moja kwa moja kwa juhudi za vita vya Urusi, na mara kwa mara wameitaka China kutumia ushawishi wake kusaidia kuleta amani nchini Ukraine.