SiasaKorea Kusini
China, Japan na Korea zakubaliana kuzidisha ushirikiano
27 Mei 2024Matangazo
Katika ujumbe wa pamoja walioutoa baada ya mkutano wa kilele mjini Seoul mataifa hayo matatu yamesisitiza dhamira yao ya kuwepo kwa Rasi ya Korea isiyo na silaha za nyuklia na suluhisho la kisiasa katika masuala kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini.
Mkutano huo wa kilele wa mataifa hayo matatu ulikuwa ni wa tisa, ila wa kwanza tangu Desemba 2019 kutokana na janga la uviko 19 pamoja na mivutano kati ya Korea Kusini na Japan.
Tangu wakati huo mahusiano baina ya nchi hizo mbili marafiki wa Marekani yameimarika.