SiasaChile
Chile yafanya kura nyingine ya maoni kubadili katiba
17 Desemba 2023Matangazo
Kura hiyo ya leo ni ya pili katika kipindi cha miaka minne iliyopita ikiwa ni juhudi za taifa hilo kubadili katiba iliyopo baada ya shinikizo kutokana na maandamano makubwa yaliyoitikisa Chile mwaka 2019.
Rasimu ya kwanza iliyojumuisha kwa sehemu kubwa misingi ya kiliberali ikiwemo usawa ndani ya jamii na haki za jinsia ilikataliwa na wapigakura mnamo Septemba mwaka jana.
Rasimu inayopigiwa kura hii leo inazingatiwa kuwa ya kihafidhana zaidi kuliko katiba ya sasa iliyoandikwa mwaka 1980 na utafiti wa maoni ya umma unaonesha huenda itakataliwa pia na wapigakura.