1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Charles III atangazwa rasmi kuwa Mfalme wa Uingereza

Sylvia Mwehozi
10 Septemba 2022

Mfalme Charles wa III ametangazwa rasmi kuwa Mfalme mpya wa Uingereza, katika sherehe zinazoendelea wakati huu na kurushwa moja kwa moja kupitia Televisheni.

https://p.dw.com/p/4GfB2
Charles III. wird feierlich zum König proklamiert
Picha: Jonathan Brady/dpa/picture alliance

Sherehe hizo zinazofanyika katika kasri la Mtakatifu James mjini London, zinahudhuriwa na baraza maalumu linahusika na kutawaza Ufalme na linaundwa na wanasiasa waandamizi na maafisa wengine washauri wa Ufalme.

Charles wa III alichukua mikoba ya Ufalme moja kwa moja mara baada ya kifo cha mama yake Malkia Elizabeth wa Pili kilichotokea siku ya Alhamis, lakini sherehe za kutawazwa ni hatua muhimu ya kikatiba ya kumtambulisha Mfalme mpya nchini humo.

Hii ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kufanyika tangu mwaka 1952 wakati Elizabeth alipotawazwa rasmi kuwa Malkia. Mfalme Charles wa III ameahidi kufuata nyayo za mama yake wakati wa hotuba yake ya kwanza aliyoitoa hapa jana. 

 

(AP)