Sayansi
Wanasayansi wawili washinda tuzo ya Nobeli ya tiba
2 Oktoba 2023Matangazo
Jopo la majaji wa tuzo hiyo limesema wawili hao wamechangia kutengenezwa kwa kasi chanjo hiyo wakati dunia ilipokabiliwa na kiticho kikubwa kwa afya ya binaadamu.
Chanjo za mRNA ziliidhinishwa kutumika mwezi Desemba mwaka 2020 na pamoja na chanjo nyengine ya Covid zikasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu na kuzuwiya magonjwa makali kwa watu wengi zaidi.
Kariko, aliye na miaka 68, na Weissman, aliye na miaka 64, waliofanya kazi kwa muda mrefu pamoja katika chuo cha Pennsylvania, Marekani wameshinda tuzo nyengine kadhaa ikiwemo tuzo ya Lasker mwaka 2021.