1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Chama tawala Serbia chatabiriwa ushindi uchaguzi wa Bunge

17 Desemba 2023

Serbia imefanya uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa leo ambao unatazamiwa kuwa kipimo kwa utawala wa rais Aleksandar Vucic na chama chake cha siasa kali cha Serbian Progressive, SNS.

https://p.dw.com/p/4aGkB
Uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa
Uchaguzi wa bunge na serikali za mitaaPicha: Jelena Djukic Pejic/DW

Licha ya upinzani mkali unaokikabili chama hicho, utafiti wa maoni ya umma unaonesha bado kina nafasi nzuri ya kupata ushindi na kuendelea kubakia madarakani. 

Inatazamiwa ushindani mkali utakuwepo kwenye wilaya za mji mkuu, Belgrade, hususani kutoka kwa wagombea wa muungano mpya wa upinzani ulioundwa miezi ya karibuni.

Vuguvugu hilo la upinzani lillopewa jina la "Serbia inayopinga vurugu" lilianzishwa kufuatia matukio mawili makubwa ya maujai ya kutumia bunduki yaliyoitikisa Serbia katikati mwa mwaka huu.

Matukio hayo yaliutia doa utawala wa Vicic ingawa mwenyewe ametoa ahadi ya kuendelea kuimarisha usalama na kupunguza mfumuko wa bei.