1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala Japan kukosa wingi wa viti bungeni

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Vyombo vya habari nchini Japan, vinatabiri kwamba chama tawala nchini humo kilichokumbwa na kashfa kitakosa wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009.

https://p.dw.com/p/4mHo2
Waziri mkuu mpya wa Japan Shigeru Ishiba
Waziri mkuu mpya wa Japan Shigeru IshibaPicha: Kyodo/AP Photo/picture alliance

Vyombo vya habari nchini Japan, vinatabiri kwambachama tawala nchini humo kilichokumbwa na kashfa kitakosa wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009, katika uchaguzi wa mapema uliofanyika Jumapili. Hatua hiyo itakuwa ni pigo kwa waziri mkuu mpya Shigeru Ishiba.

Uchunguzi wa kura za maoni unaonesha kuwa chama cha kihafidhina cha Liberal Democratic LPD na mshirika wake mdogo katika seikali, huenda wasipate wingi wa viti bungeni. Ishiba aliye na umri wa miaka  67 na waziri wa zamani wa ulinzi, aliitisha uchaguzi wa mapema baada ya kuchaguliwa kwa wingi mdogo wa kura kukiongoza chama hicho, kilichotawala Japan kwa karibu miaka 70 iliyopita. Wapiga kura katika taifa hilo la nne kiuchumi duniani wamekasirishwa na hali ya kupanda kwa bei na athari zilizochangiwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha.