SiasaMsumbiji
Upinzani nchini Msumbiji waomba kura kuhesabiwa upya
28 Oktoba 2024Matangazo
PODEMOS imechukuwa uamuzi huo baada ya kuongoza maandamano makubwa na vurugu kutokana na chama tawala cha Frelimo kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi wa rais na bunge wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizoonekana na shirika la habari la AFP, kesi iliyofunguliwa na chama cha upinzani cha PODEMOS, jana Jumapili inataka Mahakama ya Katiba kutowa uamuzi wa juu ya mshindi wa kweli wa uchaguzi huo.
Chama hicho kinaitaka mahakama itowe uamuzi wa kuhesabiwa tena kura zote, kikisema uchaguzi wa tarehe 9 ulikumbwa na dosari.
Chama hicho pia kimesema kimewasilisha ushahidi mbele ya tume ya uchaguzi,- wa maboksi kadhaa ya nyaraka zinazoonesha kilishinda uchaguzi.