1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Suu Kyi chabashiriwa ushindi Myanmar

8 Novemba 2020

Nchini Myanmar, wapiga kura Asubuhi ya leo ( 08.11.2020) wameanza kushiriki zoezi hilo, huku chama tawala la Mshindi wa Tuzo ya Nobeli,  Aung San Suu Kyi kikipewa nafasi kubwa ya kurejea madarakani.

https://p.dw.com/p/3l0yK
Wahlen in Myanmar | Vorzeitige Stimmabgabe Aung San Suu Kyi
Picha: Aung Shine Oo/AP Photo/picture alliance

Zaidi ya vyama 90 vinashiriki kuwania nafasi za uwakilishi katika bunge dogo na kubwa la taifa hilo. Kunatajwa uwepo wa zaidi ya watu miloni 37 wenye uhalali wa kupiga kura, ikiwemo idadi nyingine mpya ya wapiga kura milioni 5. Hatua hiyo inatekelezwa huku kukiwepo na hofu ya janga la virusi vya corona, huku muongozo wa kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo ukihofiwa kuathiri idadi ya watu ambao watajitokeza katika kushiriki zoezi hilo.

Kimsingi kipindi cha kampeni kilitawaliwa na hatua za kukabiliana na kitisho hicho kwa watu kukaa kwa kujitenga pamoja na uwepo wa karantini. Chama cha Suu Kyi, "National League for Democracy" kiliibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi uliopita 2015, na kuufikisha mwisho utawala wa uliokuwa ukiongozwa kwa maelekezo ya kijeshi uliodumu nchini humo kwa miongo mitano.

Suu Kyi, anasalia kuwa mwanasiasa maarufu zaidi Myanmar

Wahlen in Myanmar
Mpiga kura, baada ya kupga kura yakePicha: Aung Shine Oo/AP/picture alliance

Mpinzani mkubwa wa chama cha Suu Kyi, ni kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita, chama chenye kuungwa mkono na jeshi cha "Union Solidarity and Development", ambacho kilikuwa kinaongoza upinzani bungeni. Uwezo wa serikali ya Suu Kyi katika kuongoza nchi unatatizwa na kifungu cha kisheria ya 2008, kufuatia rasimu iliyoandikwa na jeshi, yenye kulipa jeshi hilo asilimia 25 ya viti vya ubunge, ikitoa nafasi ya kuzuia kufanyika mabadiliko ya katiba.

Suu Kyi, anasalia kuwa mwanasiasa maarifu zaidi Myanmar. Lakini serikali yake imeangukiwa katika mtazamao wa matarajio madogo, ambapo haikufanya vyema sana katika masuala ya ukuzaji wa uchumi, kukabiliana na kiwango kikibwa cha umasikini na vilevile kushindwa kupunguza msuguano unatokana na makundi hasimu ya kikabila nchini humo.

Matokeo ya uchaguzi wa Myanmar yatatangazwa Jumatatu

Kamisheni ya taifa ya uchaguzi imesema itaanza kutanga matokeo ya uchaguzi huo mapema Jumatatu. Lakini itachukua hadi wiki moja kuweza kukusanya matokeo yote, ambapo miongo mwa hayo yapo ambayo yanatarajiwa kutoka katika maeneo ya mbali na kufikika kwa shida.  Mwaka 2015 vyama vya kikabila viliungana na chama cha Suu Kyi katika kuhakikisha ushindio dhidi ya chama cha kinachoungwa mkono na jeshi cha USDP, lakini kwa uchaguzi huu vyama hivyo vimeonesha kukatashwa tamaa na kushindwa kwake kupanua wigo wa uhuru wao wa kisiasa, kwa hivyo vitaunga mkono wagomboea wao.

Soma zaidi:Xi awasili Myanamar kwa ziara ya kihistoria

Madhira ya jamii ya wachache ya Waislamu ya Rohingya ambayo imezusha wasiwasi kwa mataifa marafiki, hakuchukuliwa kwa umuhimu mkubwa katika kampeni. Mwaka 2017 kulifanyika kampeni ya kikatili ya kijeshi ambayo lilisababisha takribani watu 740,000 wa jamii hiyo kukimbia makazi yao na kwenda katika taifa jirani la Bangladesh, jambo ambalo lilisababisha uchunguzi wa kimataifa juu ya uwezekano wa kufanyika mauwaji ya halaiki.

Ubaguzi wa muda mrefu dhidi ya Warohingya, ambao wengi huwatazama kama wahamiaji haramu kutoka Asia Kusini licha ya familia zao kuishi Myanmar kwa vizazi vingi, imekuwa ikinyimwa sehemu kubwa ya haki za kiraia nchini humo,  zikiwemo haki za kimsingi, pamoja na kupiga kura.

Chanzo: APE