Chama cha MK chajiungana na upinzani Afrika Kusini
17 Juni 2024Chama chake cha cha uMkhonto weSizwe (MK) kitaungana na kile cha Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na mwanasiasa machachari Julius Malema kilichoshinda viti 39 bungeni katika bunge jipya la Afrika Kusini.
Msemaji wa MK Nhla-mulo N-dhle-la amedai licha ya matokeo ya uchaguzi huo kuchakachuliwa, vyama ambayo vitaunda muungano huo wa upinzani vilifanikiwa kupata asilimia 30 katika uchaguzi wa bunge na kulingana na msemaji huyo matokeo hayo yanawaweka katika nafasi nzuri ya kupigania ukombozi kamili wa kiuchumi wa watu weusi.
Soma pia:Biden ampongeza Ramaphosa kuchaguliwa tena Afrika Kusini
Siku ya Ijumaa MK ilisusia kikao cha kwanza cha bunge ambapo mpinzani mkuu wa Zuma Cyril Ramaphosa alichaguliwa kuwa rais wa taifa hilo kwa muhula wa pili.