1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FCC: Tshisekedi ameuvuruga uchaguzi wa Kongo

Saleh Mwanamilongo
21 Desemba 2023

Chama cha FCC (Common Front For Congo) kimesema uchaguzi mkuu wa jana Jumatano (20.12.2023) ulivurugwa huku baadhi ya raia wakilalamika juu ya dosari zilizoonekana katika uchaguzi huo.

https://p.dw.com/p/4aQzx
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Uchaguzi | Rais Felix Tshisekedi
Rais anayetetea kiti chake DR Kongo Felix TshisekediPicha: AFP

Chama hicho cha rais wa zamani Joseph Kabila, ambacho kilisusia mchakato wa uchaguzi, "kinadai Rais Tshisekedi na washirika wake katika Tume ya Uchaguzi CENI walipanga na kuhusika na vurugu hizo.

Zoezi la uchaguzi laendelea DR Kongo

Msimamo huu unafuatia ule wa wagombea watano wa Urais akiwemo Martin Fayulu na Denis Mukwege waliotaka uchaguzi uandaliwe upya na tume ya uchaguzi itakayo ridhiwa na pande zote.

Wakati huohuo CENI imeagiza kuendelea kwa uchaguzi Leo Alhamisi (21.12.2023) katika vituo ambavyo zoezi hilo halikufanyika hapo jana.

Wagombea wa upinzani Kongo walalamika kutokana na dosari za uchaguzi

Wapiga kura wanamchagua rais, wabunge na wajumbe wa serikali za mitaa. Rais aliyoko madarakani Felix Tshisekedi, anagombea muhula wa pili. Upigaji kura ulicheleweshwa kwa kiwango kikubwa hapo jana, nchini kote.

Majina yakosekana kwenye daftari

DR Kongo | Wapiga kura wakitafuta majina yao katika orodha ya wapiga kura mjini Kinshasa
Baadhi ya wapiga kura mjini Kinshasa wakitafuta majina yao kabla ya kupiga kura Picha: Mosa'ab Elshamy/AP/picture alliance

Matazizo mengi yalitokea pale wapiga kura walipokosa kuona majina yao kwenye daftari la kupigia kura.

Mjini Kinshasa vituo vya kupigia kura vilibaki wazi hadi saa tano usiku. Tume ya uchaguzi ililaumiwa kwa matatizo ya kiufundi yaliyotokea. Baadhi ya raia wanasema licha ya dola bilioni moja na laki mbili milioni ilishindwa kuaanda uchaguzi unaoaminika.

Kongo yachagua rais katikati mwa hofu ya udanganyifu

Kongo ni takriban mara nne ya ukubwa wa Ufaransa, lakini haina miundombinu ya kimsingi - hata baadhi ya miji yake kuu haijaunganishwa na barabara. Umoja wa Mataifa, Misri na nchi jirani ya Kongo-Brazzaville zilisaidia kusafirisha nyenzo za uchaguzi katika maeneo ya mbali. Lakini hata hivyo bado kunamaeneo ambayo vifaa vya uchaguzi bado kuwasili.

Watu milioni 44 wamejiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo yenye jumla ya watu milioni 100.  Matokeo ya uchaguzi yatatangazwa baada ya siku kadhaa.

Raia wa DRC wanajiandaa kumchagua rais wao