1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHADEMA watoa pendekezo la kupunguza bei ya nishati

15 Julai 2022

Licha ya serikali ya Tanzania kutoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 ili kupunguza bei ya mafuta, chama cha CHADEMA kimeitaka serikali kuondoa kodi ya shilingi 600 za Tanzania kwenye kila lita moja ya nishati ya mafuta

https://p.dw.com/p/4ED2y
Tansania | Treibstoffpreise
Picha: Yakub Talib/DW

Kauli hiyo ya kuitaka serikali kuondoa kodi ya shilingi mia sita kwenye kila lita moja ya nishati ya mafuta imetolewa na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, John Heche wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma kuhusiana na kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali nchini Tanzania hali inayowapa mzigo mkubwa watumiaji na walaji ambao ni wananchi.

Heche amesema kuwa imefika wakati sasa kwa serikali ya Tanzania kuondoa kodi ya shilingi mia sita kwa kila lita ya nishati ya mafuta ili ruzuku ya bilioni 100 iliyowekwa na serikali isaidie kupungumza mfumko wa bei za bidhaa mbalimbali zinazoelezwa kupanda nchini Tanzania.

Hata hivyo Heche ameenda mbali zaidi na kusema kuwa vita vya Ukraine sio sababu kubwa ya upandaji wa bei ya mafuta nchini Tanzania isipokuwa kuwepo kwa utitiri wa kodi kwenye bidhaa hiyo muhimu ndio sababu kubwa.

Suala la upandaji wa bei ya bidhaa mbalimbali ikiwemo nishati ya mafuta nchini Tanzania, limekuwa ni kilio kwa wananchi huku likiwaibua wachambuzi wa masuala ya uchumi kufuatia kauli ya chama cha CHADEMA. Daktari Nasibu Mramba ni muhadhiri katika chuo cha elimu ya biashara CBE cumpas ya Dodoma anasema.

Katika siku za hivi karibuni serikali ya Tanzania ilipitisha ruzuku ya shilingi bilioni 100 ili kupunguza bei ya nishati ya mafuta iliyopanda katika siku za nyuma.

Deo Kaji Makomba/Dodoma