1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANNES: Rais Chirac ataka Sudan ikubali vikosi vya kulinda amani

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRt

Rais Jaques Chirac wa Ufaransa amesema mgogoro wa Dafur ni maafa ya kibinadamu ambayo yanahatariha eneo hilo zima na ameihimiza Sudan kukubali wanajeshi wa kulinda amani huko Dafur.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa nchi na serikali wa takriban nchi 40 za Afrika Chirac amewataka wapiganaji na serikali ya Sudan kukubali uwekaji wa vikosi vya kulinda,kukomesha mashambulizi na kuwalinda raia na wafanyakazi wa misaada.

Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan na viongozi kutoka nchi jirani za Chad na Afrika ya Kati wanatazamiwa kukutana baadae leo hii pembezoni mwa mkutano huo.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambaye nchi yake inashikilia Urais wa Umoja wa Ulaya pia anahudhuria mkutano huo ambapo anawasilisha sera za Umoja wa Ulaya na Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo ya Viwanda Diniani kwa Afrika.

Katika mkutano huo Merkel pia amezitaka nchi jirani ya Zimbabwe kutumia ushawishi wao kukomesha mateso ya wananchi kutokana na sera za Rais Robert Mugabe.

Ufaransa imeamuwa kutomwalika Rais Mugabe katika mkutano huo kwa kuzingatia upigaji marufuku wa safari aliowekewa kiongozi huyo na Umoja wa Ulaya pamoja na wasaidizi wake wa karibu.