1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANNES: Al-Bashir haitaki tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan.

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRe

Rais Omar Hassan el-Bashir wa Sudan anangángánia msimamo wa kutowaruhusu nchini mwake wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Alipozungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa Ufaransa na Afrika,al-Bashir alisema kuwa katika tume hiyo ya wataalamu,kuna watu wanaopendelea upande mmoja, lakini hakueleza zaidi.Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa unataka kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la mgogoro la Darfur, magharibi mwa Sudan.Tume hiyo ilikwama Addis Ababa nchini Ethiopia kwa siku kadhaa kwa sababu Sudan imekataa kutoa vibali vya kuiwezesha tume hiyo kuingia Sudan.