Serikali ya Cameroon imerudisha huduma za mtandao wa Intaneti, baada ya kuzifungia kwa miezi mitatu katika mikoa ya kusini na kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ambako kuna watu wengi wanaozungumza lugha ya Kingereza, hatua ambayo ni moja tu kati ya nyingi zinazoashiria mpasuko na ukandamizaji uliomo ndani ya taifa hilo la magharibi mwa Afrika.