1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi yatuma wanajeshi 100 Kongo

4 Machi 2023

Burundi inatarajia kupeleka wanajeshi 100 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kama sehemu ya kikosi cha Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).

https://p.dw.com/p/4OFbG
Symbolbild I Soldaten Burundi
Picha: Mohamed Abdiwahab/AFP/Getty Images

Jumuia hiyo yenye nchi saba mwishoni mwa mwaka 2021, ilipeleka kikosi chake mashariki mwa Kongo, eneo tete ambalo linapambana na kuongezeka kwa makundi yenye silaha likiwemo kundi la waasi la M23.

Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Burundi alisema siku ya Ijumaa (Machi 3) kuwa wanajeshi wa nchi hiyo wangelielekea Goma siku ya Jumamosi.

Soma zaidi: Wabunge waitisha amani mashariki ya Kongo
Waasi wa M23 wakabiliana na jeshi la Kongo

Wanajeshi hao walitazamiwa kupelekwa Kitshanga na Kilorirwe, maeneo yanayodhibitiwa na M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini, pamoja na mji wa Sake.

Taarifa ya EAC ilithibitisha kupelekwa Kongo wanajeshi wa Burundi.

Kwa mujibu wa ratiba mpya iliyopitishwa na viongozi wa jumuia hiyo, makundi yote yenye silaha, likiwemo la M23, yanapaswa kuondoka ifikapo Machi 30, kufuatia mchakato wa hatua tatu ambao ulipaswa kuanza Februari 28.