1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Burhan amfuta kazi Dagalo kama Naibu wa Baraza Tawala Sudan

19 Mei 2023

Mkuu wa baraza la uongozi nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ametoa amri hii ya kumfuta kazi haraka iwezekanavyo kiongozi wa kikosi maalum cha wanamgambo wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo kama naibu wa baraza hilo.

https://p.dw.com/p/4RZLE
Kiongozi wa Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Sudan, Abdul Fattah al-Burhan.
Kiongozi wa Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Sudan, Abdul Fattah al-Burhan.Picha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Burhan amemteua kiongozi wa zamani wa waasi Malik Agar kuwa naibu mpya wa Baraza hilo.

Huku hayo yakiarifiwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Wakimbizi, UNHCR limesema zaidi ya watu milioni moja wameachwa bila makao kufuatia mapigano yanayoendelea Sudan.

Pande mbili hasimu za kijeshi zinazongambania madaraka zimekuwa ndani ya mgogoro kwa wiki kadhaa sasa na kusababisha mauaji ya watu wengi.

Inasemekena zaidi ya raia 250,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Chad, Ethiopia na Sudan Kusini.