1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Uturuki laidhinisha Sweden kujiunga na NATO

24 Januari 2024

Bunge la Uturuki limeidhinisha uanachama wa Sweden kwenye jumuiya ya kijeshi ya NATO baada ya kuchelewesha hatua hiyo kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4bcJD
Uturuki, Ankara, Sweden, NATO
Bunge la Uturuki limeidhinisha uanachama wa Sweden kwenye Muungano wa Kijeshi wa NATO.Picha: Ali Unal/AP Photo/picture alliance

Wabunge 287 waliunga mkono hatua hiyo na 55 waliipinga.

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki anatarajiwa kutia saini ridhaa hiyo ya kuiingiza Sweden kuwa mwanachama wa 32 wa NATO.

Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson amesema kwenye mtandao wa kjamii kwamba nchi yake imesonga mbele zaidi katika hatua ya kuwa mwanachama kamili wa NATO.

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ameukaribisha uamuzi wa Uturuki na ametoa wito kwa Hungary ichukue hatua kama ya Uturuki.

Marekani pia imesifu uamuzi wa bunge la Uturuki.