1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Uturuki kuidhinisha uanchama wa Sweden NATO

23 Januari 2024

Kura ya kuiidhinisha Sweden kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO imepangwa kufanyika katika bunge la Uturuki baada ya miezi mingi ya shinikizo kutoka kwa washirika wa NATO.

https://p.dw.com/p/4ba7p
Uturuki Ankara | Bunge kuidhinisha uanachama wa Sweden NATO
Bunge la Uturuki likiendelea na vikao vyake mjini AnkaraPicha: Hakan Nural/AA/picture alliance

Kura hiyo ipo katika ajenda ya bunge la Uturuki hii leo, lakini muda haswa itakapopigwa kura hiyo bado haujajulikana.

Iwapo Uturuki itaiidhinisha Sweden kujiunga na jumuia hiyo, Hungary ndiyo itakuwa nchi pekee mwanachama wa NATO ambaye haijaiidhinisha Sweden kujiunga na muungano huo wa kijeshi.

Soma pia: Katibu Mkuu wa NATO atumai Sweden itakuwa mwanachama Julai 2024

Kila mwanachama wa NATO anapaswa kutoa ruhusa ili Sweden iweze kujiunga. Kamati ya mambo ya kigeni ya bunge la Uturuki tayari ilipiga kura kuiruhusu Sweden kujiunga na NATO.

Kitisho cha kutanuka kwa uvamizi wa Urusi kutokana na vita vyake nchini Ukraine, kiliisukuma Sweden na Finland kuomba kujiunga na NATO. Finland ilijiunga na jumuia hiyo mwezi Aprili, mwaka uliopita.