1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ukraine kulihutubia Bunge la Uswisi.

6 Mei 2023

Bunge la Uswisi limeridhia ombi la mamlaka za Ukraine la kumruhusu Rais Volodymyr Zelensky kulihutubia. Tangazo la mwaliko huo wa kulihutubia bunge lilitolewa Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4QzBU
Ukraine Präsident Wolodymyr Selenskyj
Picha: president.gov.ua

Bunge la Uswisi limeridhia ombi la mamlaka za Ukraine la kumruhusu Rais Volodymyr Zelensky kulihutubia. Tangazo la mwaliko huo wa kulihutubia bunge lilitolewa Ijumaa wakati kukiwa na shinikizo la kuitaka serikali ya Uswisi kuvunja utamaduni wake wa muda mrefu wa kutokuegemea upande wowote. Uswisi inakabiliwa pia na shinikizo la kutakiwa kukomesha kuuza silaha kwa maeneo yenye mizozo kama Ukraine ingawa hadi sasa serikali hiyo imekataa kubadilisha sera hiyo. Hotuba ya Zelensky itakakuwa ya kwanza kutolewa na kiongozi huyo kwa njia ya video. Bunge la Uswisi linatarjiwa kuanza vikao vyake mnamo Mei 30. Wabunge wa Uswisi pia watajadili hoja juu ya nchi yao kuipa Ukraine msaada wa dola bilioni 5.6 kwa kipindi cha miaka 5 hadi 10.