Bunge la Ujerumani laidhinisha bajeti kubwa kwa jeshi
19 Oktoba 2023Matangazo
Waziri wa Masuala ya Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, aliitaja hatua hiyo ni ishara ya kuwa wanaishi katika nyakati mpya.
Mradi mkubwa ulioidhinishwa unahusu ununuzi wa mfumo wa ulinzi wa anga kutoka Israel na karibu dola bilioni 4 ni katika fuko maalum.
Soma zaidi: Jeshi la Ujerumani linakabiliwa na ugumu wa kupata askari wapya
Kansela Olaf Scholz alisema mnamo mwezi Februari kwamba uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine vilisababisha hatua ya mageuzi na uwekezaji mkubwa katika jeshi.
Aliahidi kuongeza matumizi kwa zaidi ya asilimia mbili ya pato jumla na kuongeza Ujerumani pia itaanzisha fuko maalum litakalofadhiliwa kwa gharama za bilioni Euro 100 kwa ajili ya kuboresha jeshi lake, Bundeswehr.