Bunge la Ujerumani latambua mauaji ya Wayazidi ya mwaka 2014
19 Januari 2023Matangazo
Katika hatua iliyopongezwa na wawakilishi wa jamii hiyo ya Wayazidi, wabunge katika bunge hilo wameupitisha muswada huo. Bunge hilo limesema limechukua hatua hiyo kufuatia tathmini ya kisheria iliyofanywa na Umoja wa Mataifa. Ujerumani inafuata nyayo za nchi nyengine kama Australia, Ubelgiji na Uholanzi kuyatambua mauaji hayo kama mauaji ya halaiki. Bunge la Ujerumani limesema uhaini uliofanywa na wanamgambo wa Dola la Kiislamu ulikuwa na lengo la kuiangamiza kabisa jamii ya Wayazidi.