Bunge la Namibia kujadili makubaliano ya fidia ya Ujerumani
22 Septemba 2021Matangazo
Majadiliano ya bunge nchini Namibia kuhusu makubaliano kati ya nchi hiyo na Ujerumani kulipa fidia kwa wahanga wa mauaji ya kimbari ya wakati wa ukoloni wa kijerumani ambayo bado hayajasainiwa, yanatarajiwa kuanza tena Jumatano.
Spika wa Bunge, David Nahongandja amesema siku ya Jumatano kuwa ana matumaini kura inaweza ikafanyika katika siku zijazo.
Kura hiyo imecheleweshwa baada ya vikao vya bunge kuahirishwa mwezi Juni kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Kwa mujibu wa Nahongandja, wabunge wa upinzani mara kwa mara waliizuia serikali kuwasilisha makubaliano hayo bungeni hapo jana.
Takribani watu 300 waliandamana nje ya jengo la bunge kupinga makubaliano yaliyopendekezwa.