1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Bunge la Marekani lagawika juu ya usaidizi kwa Ukraine

3 Novemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amelitaka bunge la Marekani, liupitishe haraka muswada wa mabilioni ya dola ya misaada mipya kwa Israel na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4YJGf
Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden Picha: Andrew Harnik/AP/dpa/picture alliance

Lakini Baraza la Wawakilishi ambalo linadhibitiwa na Warepublican, linatarajiwa kuzingatia muswada ambao hauijumuishi Ukraine.

Wabunge wa chama cha Democratic na Warepublican wote kwa pamoja wanataka kuupitisha muswada wa misaada kwa Israel ambayo kwa muda mrefu imekuwa mshirika wa Marekani katika vita dhidi ya Hamas ila tofauti inakuja linapoingia suala la msaada zaidi kwa Ukraine.

Umoja wa Ulaya watofautina kuhusu msaada Ukraine

Wahafidhina wachache wenye misimamo mikali katika baraza la wawakilishi, wanataka msaada kwa Ukraine usitishwe kabisa.

Marekani imekuwa nchi inayotoa msaada wa kiasi kikubwa kwa Ukraine tangu Urusi kuivamia Februari mwaka jana 2022.

Lakini ahadi ya Rais Biden kwa Rais Volodymyr zelenskiy inaonekana kuwa mashakani sasa.