Bunge la Marekani kupigia kura miswada ya msaada
20 Aprili 2024Kura ya miswada hiyo ya takribani dola bilioni 95 za msaada kwa mataifa ya kigeni pamoja na ununuzi wa silaha inatarajiwa kupigwa baadaye leo, huku Spika Mike Johnson wa chama cha Republican akihitaji uungwaji mkono wa chama cha Democrat kuipitisha.
Soma pia: Marekani yaihakikishia Ukraine kupata msaada wa kijeshi
Miswada hiyo inatokana na mchakato wa miezi kadhaa ya majadiliano na shinikizo kutoka kwa washirika wa Marekani pamoja na maombi ya mara kwa mara ya msaada kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.
Marekani haijaidhinisha msaada mkubwa kwa Ukraine kutokana na mvutano wa kisiasa
Marekani imekuwa mfadhili mkubwa wa kijeshi kwa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi, lakini bunge la nchi hiyo halijaidhinisha msaada wa kiwango cha juu kwa taifa hilo kwa takribani mwaka mmoja na nusu kutokana na mvutano wa kisiasa.