Haki za binadamuGhana
Bunge la Ghana limepiga kura kufuta adhabu ya hukumu ya kifo
26 Julai 2023Matangazo
Kulingana na ripoti ya kamati ya bunge, muswada huo mpya unalenga kurekebisha Sheria ya Makosa ya Jinai, ambapo nafasi ya adhabu ya kifo sasa itakuwa kifungo cha maisha jela. Ili ianze kutekelezwa, sheria hiyo lazima kwanza iidhinishwe na Rais Nana Akufo-Addo.
Hatua hiyo ni maendeleo makubwa kwa haki za binadamu
Mbunge Francis-Xavier Sosu, aliyewasilisha muswada huo ameielezea hatua hiyo kama maendeleo makubwa ya rekodi ya haki za binaadamu nchini Ghana. Idara ya Magereza nchini Ghana imesema hakuna mtu ambaye amenyongwa nchini humo tangu mwaka 1993. Hata hivyo, watu 176 walikuwa wamehukumiwa kifo hadi mwaka jana.