1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaFinland

Bunge la Finland lapiga kura kwa wingi kujiunga na NATO

1 Machi 2023

Bunge la Finland limepiga kura kwa wingi ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, kuelekea idhinisho la Hungary na Uturuki. Hatua hiyo inaongeza uwezekano kuwa itajiunga na Jumuiya hiyo kabla jirani yake Sweden

https://p.dw.com/p/4O7ke
Finnland | Abstimmung zum NATO Beitritt im Parlament in Helsinki
Picha: Heikki Saukkomaa/AP Photo/picture alliance

Wabunge 184 wamepiga kura ya kukubali masharti ya NATO dhidi ya saba waliopinga. Bunge la Finland limehakikisha kwamba sheria hiyo inapitishwa kwa haraka kuelekea uchaguzi mkuu wa Aprili 2 ili kuepuka masuala ya uidhinishaji yaliyopo kabla serikali mpya kuchaguliwa.

Soma pia: NATO yasema wakati ni sasa wa kuruidhia maombi ya Finland na Sweden kujiunga na jumuiya hiyo

Finland na Sweden zote ziliacha sera zao zilizodumu kwa miongo kadhaa ya kutokuwa wanachama wa miungano ya kijeshi na kuwasilisha maombi ya kujiunga na NATO mwei Mei mwaka jana, baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Ingawa Sweden imekuwa na migongano kadhaa ya kidiplomasia na Uturuki ambayo ni mwanachama wa NATO ambayo imetishia kuchelewesha ombi lake la uanachama na kujiunga kwa wakati mmoja na Finland.