JamiiAlgeria
Bunge Algeria laidhinisha sheria mpya ya vyombo vya habari
14 Aprili 2023Matangazo
Ijapokuwa serikali imesema sheria hiyo ni muhimu kwa kuimarisha uhuru wa shughuli za vyombo vya habari, asasi ya kimataifa ya waandishi wasio na mipaka RSF imesema sheria hiyo mpya inajumuisha vipengele vinahujumu uhuru huo.
Sehemu ya sheria hiyo inapiga marufuku kwa vyombo vya habari vya Algeria kupokea misaada ya kifedha au vifaa vya kazi kutoka nje. Pia inaweka zuio kwa watu wenye uraia pacha kuwa na haki ya kumiliki au kuwa sehemu ya umiliki wa vyombo vya habari nchini Algeria.
Pamoja na vifungu vya aina vinavyotiliwa shaka, sheria hiyo itarahisisha mchakato wa kufungua magazeti na majarida na kuachana na utaratibu wa hapo kabla wa kuomba kibali kutoka wizara ya mawasiliano ya nchi hiyo.