1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Brussels yatangaza tahadhari ya tishio la kigaidi

17 Oktoba 2023

Tahadhari ya hali ya juu zaidi ya kitisho cha ugaidi imetangazwa katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.

https://p.dw.com/p/4Xbu2
Maafisa wa polisi wanamtafuta mshambuliaji.
Maafisa wa polisi wanamtafuta mshambuliaji.Picha: Sylvain Plazy/AP/picture alliance

Ni baada ya mshambuliaji ambaye hajatambuliwa kuwaua watu wawili kwa kuwapiga risasi usiku wa kuamkia leo Jumanne.

Kulingana na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander De Croo, waliouawa kwenye shambulizi hilo ni raia wawili wa Uswidi.

Kituo cha Ubelgiji cha kushughulikia migogoro kimesema hayo kupitia ukurasa wake wa X ambayo zamani ilijulikana kwama Twitter.

Kulingana na kituo hicho, kiwango cha 4 cha kitisho kimetangazwa katika eneo zima la mji mkuu.

Waziri wa ndani wa Ubelgiji Annelies Verlinden ameandika kwenye ukurasa wake wa X kwamba msako dhidi ya mshambuliaji unaendelea.

Mechi ya kufuzu Kombe la Euro 2024 kati ya Uswidi na Ubelgiji, iliyokuwa ikichezwa wakati shambulizi lilipotokea iliahirishwa.