Gabon: Jenerali Nguema ateua wapinzani kuongoza serikali
12 Septemba 2023Wakati huo huo, Nguema amemteua Jean Francois Ndongou, aliyeshikilia nyadhifa mbalimbali za uwaziri chini ya utawala wa Bongo, kuwa spika wa bunge la kitaifa.
Nguema, aliyetangazwa kuwa rais wa mpito, aliongoza mapinduzi yasiyo na umwagaji damu yaliyomuondoa madarakani Ali Bongo Ondimba mnamo Agosti 30.
Soma pia:Utawala wa kijeshi Gabon wamemteua kiongozi wa upinzani kuwa Waziri Mkuu wa mpito
Jenerali huyo wa jeshi ameahidi kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kiraia na kufanyika kwa uchaguzi baada ya kipindi cha mpito japo hakuweza wazi tarehe maalum ya hilo kufanyika.
Tayari ameunda serikali ya mpito chini ya waziri mkuu mpya Raymond Ndong Sima, mchumi aliyesoma nchini Ufaransa na aliyewahi kuhudumu kama waziri mkuu chini ya utawala wa Bongokutoka mwaka 2012 hadi 2014 kabla ya kushindana naye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 na 2023.