Brazil yarekodi vifo vya kwanza vilivyotokana na Oropouche
26 Julai 2024Wizara ya afya nchini Brazil imesema wanawake hao kutoka jimbo la Bahia kaskazini mashariki mwa Brazil walikuwa chini ya umri wa miaka 30 na walionyesha dalili za homa kali ya dengue.
Wizara hiyo imeongeza kuwa, imeorodhesha wagonjwa 7,236 waliokutwa na virusi vya Oropouche mwaka huu pekee japo wengi wameripotiwa kutoka majimbo ya Amazonas na Rondonia.
Soma pia: Tanzania yakiri kuwa na Chikungunya, Dengue
Tovuti ya kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani imeeleza kuwa, kuna mripuko wa ugonjwa wa Oropouche nchini Bolivia, Brazil, Colombia, Cuba na Peru.
Dalili za mgonjwa wa Oropouche hufanana na homa ya dengue na hudumu kati ya siku tatu hadi sita. Dalili hizo ni pamoja na maumivu ya misuli, viungo, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutapika na mgonjwa kuhisi baridi mwilini.