1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brahimi akutana na Muallem

30 Oktoba 2013

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Syria, Walid Muallem, amesisitiza kuwa ni Wasyria pekee ambao wanawajibu wa kuchagua hatima yao na amepinga madai ya mataifa ya Magharibi kuwa Rais Bashar al-Assad ajiuzulu.

https://p.dw.com/p/1A8yD
epa03439649 Syrian Foreign Minister Walid al-Moallem(R) meets with Lakhdar Brahimi, the joint UN-Arab League envoy, in Damascus, Syria, 20 October 2012. Brahimi flew in a day earlier to push for his plan to achieve a cease-fire during the four-day Eid al-Adha holiday that begins on 26 October. Brahimi has said he has no grand plan to end Syria_s civil war. Instead, he presented the truce as a 'microscopic' step that would alleviate Syrian sorrow temporarily and provide the basis for a longer truce. EPA/YOUSSEF BADAWI +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa mambo ya kigeni wa Syria Walid al-Muallim(kulia) na Lakhdar BrahimiPicha: picture-alliance/dpa

Muallem alisema hayo wakati akizungumza na mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Mataifa ya Kiarabu, Lakhdar Brahimi, ambaye anajaribu kutafuta uungwaji mkono wa mazungumzo ya amani mjini Geneva.

Syria itashiriki katika mazungumzo ya Geneva katika msingi wa haki kamili za Wasyria kuchagua mustakabali wao wa kisiasa, kuwachagua viongozi wao na kutupilia mbali aina yoyote ya uingiliaji kutoka nje, amesema waziri huyo wa mambo ya kigeni Walid Muallem.

Pia amesema kuwa maelezo yote juu ya hali ya baadaye ya nchi hiyo, hususan matamshi kutoka mjini London, yanakiuka haki ya watu wa Syria.

Source News Feed: EMEA Picture Service ,Germany Picture Service International peace envoy for Syria Lakhdar Brahimi arrives at his hotel in Damascus December 23, 2012. Brahimi is expected to meet Syrian President Bashar al-Assad a day later, airport sources in Lebanon said. REUTERS/Khaled al-Hariri (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Lakhdar BrahimiPicha: Reuters

Hii ni kwa mujibu wa mkutano uliofanyika Oktoba 22 wa kile kinachojulikana kama "Marafiki wa Syria", kundi la mataifa, ambayo yanaunga mkono upinzani nchini Syria.

Katika mkutano huo, mataifa ya magharibi na yale ya Kiarabu yalikubaliana na viongozi wa upande wa upinzani kuwa Assad hana nafasi katika uongozi wa hapo baadaye nchini humo kama alivyoeleza waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, William Hague.

"Assad hatakuwa na wajibu wowote katika utawala mpya wa Syria."

Lakhdar kukutana na Assad

Leo hii (30.10.2013)mjumbe wa Umoja wa Mataifa na mataifa ya Kiarabu Lakhdar Brahimi atakutana na rais wa Syria Bashar al-Assad mjini Damascus, zimesema duru za kidiplomasia. Utakuwa ni mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu pale Brahimi alipozuru nchini humo Desemba mwaka jana.

British Foreign Secretary William Hague speaks to journalists following a meeting with Palestinian President on May 23, 2013 in the West Bank city of Ramallah. Peace between Israel and the Palestinians is a "priority," Hague said on a visit to the region, as he met Israeli Prime Minister earlier in the day. AFP PHOTO/ ABBAS MOMANI (Photo credit should read ABBAS MOMANI/AFP/Getty Images)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William HaguePicha: ABBAS MOMANI/AFP/Getty Images

Wakati huo huo, karibu Wasyria 2,000 wamekimbia kutoka katika wilaya iliyokumbwa na mapigano mjini Damascus ya Moadamiyeh jana kwa msaada wa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada wakati wa muda mfupi wa kusitisha mapigano, ikiwa ni matokeo ya makubaliano ambayo ni ya nadra kati ya majeshi ya serikali na waasi katika hatua ya kuepusha hali mbaya ya mzozo wa kibinaadamu.

Njaa na magonjwa

Hatua hiyo imewezekana baada ya ripoti za ukosefu wa chakula na njaa pamoja na magonjwa katika kitongoji cha magharibi mwa mji huo baada ya miito ya jumuiya ya kimataifa.

Nalo shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limethibitisha jana kuwa umezuka ugonjwa wa polio katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita, ambayo ilikuwa haina ugonjwa huo tangu mwaka 1999, na shirika hilo limesema linahofia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Mwandishi: Sekione Kitojo/afpe/ape
Mhariri: Josephat Charo